Tuesday, 3 July 2012
NAKAAYA ALIA KWA KUPOKONYWA BWANA
MWANAMUZIKI Nakaaya Sumari, juzikati alimwaga machozi huku akidai kuibiwa bwana’ke na mwanamke mwenzake aliyemtaja kwa jina la Beatrice, Ijumaa linakupa mchapo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Nakaaya amekuwa hana raha baada ya kuzidiwa ujanja na Beatrice ambaye inadaiwa ni mzazi mwenza wa mwanaume huyo anayetajwa kwa jina la Peter.
“Yaani Nakaaya hana raha kabisa baada ya kuchukuliwa bwana wake. Lakini sisi uhusiano wake na Peter hatukuwa tunaujua na inaonekana walikuwa wakitoka kwa siri sana,” alisema sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake .
Ijumaa lilipozinasa habari hizi lilimwendea hewani msanii huyo ambaye alipopatikana alitoa ushirikiano kwa paparazi wetu akisema:
“Ni kweli kumetokea msuguano kati yangu na Peter ambaye nilikuwa nampenda sana na tukadumu kwa miaka miwili, lakini niligundua amempa mimba mwanamke mwingine,” alisema Nakaaya na kuongeza:
“Mimi sitaki shari naye kwa kuwa tabia yake haijanifurahisha, nina mambo mengi ya kufanya kama Peter bado anamzimia basi waendelee ila Beatrice asiwe ananisumbua maana nimechoka na mapenzi ya kushea bwana, bora nizame kwenye game la muziki kama mwanzo,” alisema Nakaaya.
Kwa upande wa Peter, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alikiri na kusema kuwa ameamua kuendeleza uhusiano wake na Beatrice ambaye yuko naye kwa zaidi ya miaka mitano baada ya kuona Nakaaya haelekei.
“Nilikuwa nampenda sana Nakaaya lakini nimeshindwa baada ya kusikia ana bwana mwingine wa Kizungu, nisingeweza kuendelea naye bora niendelee kudili na kazi zangu na maisha mengine, mapenzi ya ki-supastaa yamenishinda,” alisema Peter.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment