Wednesday, 11 July 2012

UTUNDU AMA UTOVU?





CHIPUKIZI anayekuja kwa kasi kwenye soko la filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kwa mara nyingine anatengeneza kichwa cha habari baada ya kufanya uchafu huku akishuhudiwa na watu, Risasi Mchanganyiko linakufunulia.
Madudu ya Vai yalinaswa laivu na kamera yetu, wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Motema uliopo Mwananyamala, Dar ambapo kulikuwa na ‘birthday’ ya msanii huyo.
Mbele ya macho ya watu, bila kujali kuna waliomzidi umri, Vai alikuwa karibu sana na mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Boniface ambaye alitambulishwa kama boyfriend wake na kuanza kudendeka naye bila aibu.
Aidha, kuna wakati alikamatana na baadhi ya rafiki zake wa kike na wa kiume (wanaodaiwa ni kuku watamu) na kuanza kudendeka kama alivyofanya kwa Boniface.
Kama hiyo haitoshi, Vai alifikia hatua ya kupandisha gauni lake juu na kuacha ‘kufuli’ lake nje kama vile alikuwa bafuni (angalia picha ukurasa wa nyuma).
Watu wenye heshima zao walibaki vinywa wazi na kugeuza nyuso kukwepa aibu ya msanii huyo ambaye anaonekana kuamini kufanya uchafu ndiyo kupata ustaa.



No comments:

Post a Comment