Monday, 25 June 2012
LAIVU!
MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa picha za utupu na kusambazwa kila kona ya jiji.
Picha hizo zinamuonesha Jack akiwa kama alivyozawaliwa katika mapozi tofauti, jambo ambalo linaonesha kuwa alipigwa picha hizo na mpenzi wake.
Kikizungumza na Risasi Mchanganyiko, chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu na msanii huyo, kilisema Jack amekuwa akilalamika kuhusu kupotelewa na kadi iliyokuwa na picha zake za siri hivyo inawezekana aliyechukua ndiyo amezisambaza picha zisizofaa kuonekana hadharani.
“Kwa pozi hili aliloweka Jack inawezekana alipigwa na mpenzi wake kwa lengo la kujifurahisha kama wapenzi, mapozi aliyokaa yanathibitisha hilo kabisaa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzitia picha hizo kibindoni, gazeti hili lilimtafuta Jack ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Jamani hizo picha sielewi zimevujaje maana kuna kadi yangu ya simu ilipotea ikiwa nazo, nilipigwa na mpenzi wangu kwa nia njema tu, si unajua mambo ya mapenzi tena… sasa kama zimeshafika kwenu sijui niseme nini tena hapo.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment